2 Chronicles 5:1-6

1 aHivyo Sulemani alipomaliza kazi ya Hekalu la Bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani, fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.

Sanduku La Agano Laletwa Hekaluni

(1 Wafalme 8:1-9)

2 bKisha Sulemani akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 3 cNao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu mwezi wa saba.

4 dWazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano, 5 enao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo, 6naye Mfalme Sulemani na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ng’ombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa.

Copyright information for SwhKC